26 Aprili 2015 - 12:39
Mauaji dhidi ya taifa la Yemen bado yaendelea

Vyombo vya habari vyaripoti kufanywa milipuko mikubwa katika mji mkuu wa Yemen Sana`a kutokana na makombora yanayopigwa na ndege za kijeshi za Saudi Arabia nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwamujibu wa tovuti ya Almotamar net ni kwamba ndege za kivita za Saudi Arabia na washirika wake usiku wa Jumapili umefanya mashambulizi makali ya mabomu katika mji mkuu wa Yemen Sana`a nakusababisha maafa makubwa nchini humo.
Mashambulio hayo yalifanyika katika maeneo ya Fag Attan na sehemu zingine tano mjini Sana`a ambapo yalipelekea kusikika sauti kubwa ya milipuko katika semehizo mbalimbali za mji huo.
Wakazi wa mji mkuu wamesema kuwa kutokana na uzito wa sauti za milipuko hiyo imepelekea vioo kuvunjika nakuharibu madirisha ya majengo mengi mjini Sana`a, huku wakibainisha kuwa mpaka sasa idadi ya watu waliopoteza maisha katika mashambulio hayo bado.
Mashambulizi ya ndege za Saudi Arabia yaingia mwezi wa pili sasa toka yalipoanza tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu, pamoja kuwa serikali hiyo ilitangaza kusitisha mashambulizi yake nchini humo.
Vyombo vya habari mbalimbali vimedhibitisha kutokea kwa mashambulizi hayo huku vikisisitiza kuwa mashambulio hayo yalikuwa yanalenga kuharibu makao makuu ya kusambaza maji katika mji huo.
Ndege hizo za Saudi Arabia pia zilishambulia malori yaliobeba misaada ya kibinadamu kwaajili ya wananchi waliokuwa katika hali mbaya nchini humo, pia ndege hizo zilishambulia kambi ya jeshi ya Dhabaani iliopo Taez.
baada ya kupita siku 27 za mashambulizi ya utawala wa Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen utawala huo siku ya Jumatano iliopita ulitangaza kusitisha mashambulizi hayo, ama baada masaa mawili kupita ndege za Saudi Arabia ziliendeleza kufanya mashambulizi ya anga nchini humu katika sehemu mbalimbali nchini Yemen ikiwemo kambi ya Alastqbal iliopo kaskazini mwa mji mkuu Sana`a.